Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Javad Naqavi, Rais wa Harakati ya Uamsho wa Umma wa Mustafa wa Pakistan, wakati wa maadhimisho ya siku ya “Mafufirko ya Al-Aqsa”, alisisitiza umuhimu wa kuadhimisha tarehe 7 Oktoba kama siku ya kuliweka hai Suala la Palestina, kutangaza mshikamano na watu wanaodhulumiwa wa ardhi hiyo na kuimarisha uamsho wa Umma wa Kiislamu.
Amesema: Operesheni ya “Mafuriko ya Al-Aqsa” kwa mara nyingine iliweka Suala la Palestina katika uangalizi wa kimataifa, na sasa ni jambo la lazima tarehe 7 Oktoba ibadilishwe kuwa fursa ya kuwaunga mkono watu wanaodhulumiwa wa Palestina na kupinga vitendo vya Israel na Marekani.
Rais wa Harakati ya Uamsho wa Umma wa Mustafa wa Pakistan ameongeza: Suala la Palestina na Ghaza haliwahusu watu wa Palestina pekee, bali ni suala linalouhusu Umma wote wa Kiislamu na kila mwanadamu mwenye ufahamu na aliye huru. Kwa hiyo, inapaswa kutangazwa mshikamano na watu wanaodhulumiwa wa Palestina na kuungwa mkono kwao Muqawama kwa kuandaa maandamano, mikusanyiko na programu mbalimbali katika maeneo yote ya Pakistan.
Akizungumzia ukimya wa baadhi ya serikali za Kiislamu na utendaji dhaifu wa taasisi za kimataifa kuhusiana na mgogoro wa Palestina, amesema: Kuendelea hali hii kumeongeza ukubwa wa janga la Palestina. Umma wa Kiislamu haupaswi kuuwekea mipaka msaada wake kwa Palestina katika kulaani na kutoa taarifa pekee, bali unapaswa kuchukua hatua za kivitendo na zenye ufanisi kwa ajili ya kuwaunga mkono watu wa Palestina na kutetea haki zao.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Javad Naqavi amesisitiza mwishoni: Tarehe 7 Oktoba inapaswa kubadilishwa kuwa siku ya kuliweka hai Suala la Palestina, kusimama pamoja na waliodhulumiwa na kueneza ujumbe wa uamsho miongoni mwa Umma wa Kiislamu.
Maoni yako